1 Aprili 2025 - 16:52
Mashambulizi ya roketi kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu

Makazi ya Wazayuni ya "Sadirot" yalilengwa kwa shambulio la roketi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Makazi ya Wazayuni ya "Sadirot" karibu na Ukanda wa Gaza yalilengwa na mashambulizi ya roketi ya makundi ya Muqawama wa Palestina saa moja iliyopita.

Kengele ya hatari ilisikika katika mji wa Sadirot na mazingira yake baada ya shambulio hili la roketi na Wazayuni wanaoishi katika mji huu walilazimika kuingia ndani ya makazi / ngome zao za kujihami.

Vikosi vya Quds, tawi la kijeshi la harakati ya Jihad ya Kiislamu ya Palestina, walitangaza kuhusika na kuwajibika kwa shambulio hili la roketi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Jeshi la Israel linadai kuwa mifumo yake ya ulinzi ilinasa roketi iliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Saderot.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha